"MWADVENTISTA NA SIASA"JE NI SAWA KUWA MWANASIASA HUKU IKIWA MWADVENTISTA?


NI KIPINDI MAALUM CHA MJADALA KILICHOHUDHURIWA NA WAUMINI WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO TOKA NDANI NA NJE YA VIUNGA VYA JIJI LA MWANZA KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KIRUMBA MWANZA TANZANIA.
BAADHI YA WATU MASHUHURI WALIOSHIRIKI MJADALA HUO NI MH. STEPHEN MAGOIGA, MFAMASIA NA MWINJILISTI PHILIPO JOSEPH, NDUGU MECK MANYAMA,MZEE SITTA NGISSA, NDUGU SAMUEL NKONYA, NDUGU JOSEPH NJILE,DR.ONDITI, DR. PRAYGOD NA WENGINE WENGI KWA USIMAMIZI WA MCHUNGAJI BEATUS MLOZI.
HATA HIVYO BAADA YA MAJADILIANO MAREFU TULIHITIMISHA KWA KUKUBALIANA YAFUATAYO:-
Sheria ya Mungu katika ulimwengu imejengwa katika utayari wa utii wa viumbe vyake alivyoviweka kwa ukarimu wake mkuu. Ni imani pekee ndiyo iliyosimikwa katika moyo wa mwanaadamu na kutegemeza kila tendo litakalosukumwa na upendo wake. Hakika hilo ndilo linalokubalika na Mungu. Upendo hata hivyo siyo msingi wa sheria za serikali. Kwa hiyo juhudi za kushinikiza imani kwa asili yake ni kinyume na dini ya kweli, na hili ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
Kama Waadventista wa Sabato tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na serikali zilizosimikwa katika jamii zetu. Tunapaswa kuziheshimu na kuziunga mkono kwa juhudi zote zinapokuwa katika harakati za kutekeleza majukumu yake. Ila pale tu itakapoonekana ya kuwa sheria ya nchi mahalia inapingana na mamlaka ya neno la Mungu, tunapaswa kusimama katika neno , maana ni bora kumtii Mungu kuliko mwanadamu. Waadventista wa Sabato tumeitwa kusimamia kanuni za uhuru wa dhamiri wakati wote tukiendelea kuwapenda na kuwathamini wengine.
Kanisa la Waadventista wa Sabato linatambua historia ndefu inayoonyesha namna watu wa Mungu walivyoshika madaraka na kushiriki katika shughuli za kiserikali. Yusufu alikuwa na madaraka ya kiserikali katika nchi ya Misri, vivyo hivyo Daniel, alipanda vileleni kimamlaka katika Babeli na matokeo yake taifa likafaidi kwa uwepo wao.
Kimsingi mivuto ya kisiasa si tatizo, Muadventista anaweza kujisikia kushikilia madaraka katika uongozi katika serikali, hata hivyo siku zote tunapaswa kuwa makini kwa hatari ambazo zinaambatana na mivuto ya kidini katika utendaji wa serikali na kudumu bila kuchoka kukwepa kwa makini hatari hizo.
Kila inapotokea Muadventista wa Sabato kuwa kiongozi, akitoa mvuto wake katika jamii anapaswa kufanya hivyo kwa kutumia kanuni ya dhahabu (Golden rule).
Tunapaswa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupiga kura unaopatikana katika maeneo yetu. Ikiwa inawezekana kufanya hivyo, basi tushiriki katika dhamiri safi na kuwajibika kikamilifu (GW 391, 392)
Waadventista wa Sabato hatupaswi kubobea katika masuala ya siasa na kuzitumia mimbari zetu au machapisho yetu kusukuma utawanyaji wa mawazo ya kisiasa.
Waadventista ambao ni viongozi serikalini wanapaswa kukubali na kuazimia kuweka maishani viwango vya juu vya maisha ya kikristo. Wawe akina Daniel wa kisasa na Bwana atawaongoza kutenda mapenzi yake na kuisaidia jamii kumjua Mungu.
Maonyo mazito yametolewa na Mama E. G. White dhidi ya masuala ya kisiasa na shughuli zake amesema, “Acha kabisa masuala ya siasa……. Kila mwalimu, Mchungaji au kiongozi katika ngazi za kanisa ambaye ana kusudia kupenyeza mawazo yake katika masuala ya siasa anapaswa kurejeshwa katika kuiamini kweli ama sivyo ajiuzulu katika wadhifa aliopewa” (GW 392, 393)
<IWAPO UMEBARIKIWA SEMA AMINA>

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright ©2015 KIRUMBA ADVENTIST CHURCH