“Mimi ni nani, hata niwahukumu mashoga?”
Conges Mramba na Mashirika ya Habari
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani,Papa Francis amehitimisha ziara
yake katika nchi tatu za Afrika zinazokabiliwa na hatari ya vita na
Ugaidi,Kenya,Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati(CAR),huku akiagiza haki
za watu wote(wakiwemo mashoga)kulindwa na kuheshimiwa.
Akiwa
Afrika ya Kati,Papa Francis amesema anatazamia kuona kila jamii inapewa
haki bila kuachwa kundi lolote wakiwemo wapenzi wa jinsi moja-mashoga na
wasagaji.
Msemaji wa Vatican,Father Federico Lombardi,amesema
ingawa Papa hakutaja mashoga,lakini kauli yake ililenga hata wapenzi wa
jinsi moja- homosexuals- haki zao kulindwa na kuheshimiwa.
Wakati
wa ziara hii ya Papa Barani Afrika,wanaharakati wa haki za mashoga
wamemwomba Papa kutangaza kwamba sheria kali dhidi ya mashoga katika
nchi za Afrika ni haramu na hazifai kabisa.
Msemaji huyu wa Vatican amesema Papa hakukusudia kujihusisha chochote na mashoga katika ziara hii ya Afrika.
Jijini Kampala,Kiongozi huyu wa Kanisa Katoliki alikutana na vijana na
wakimbizi, yatima na hata walemavu alipokuwa uwanja wa ndege.
Kwa
muda mrefu sasa Papa amekuwa na msimamo unaoenda sambamba na
kinachoitwa na Ulaya na Marekani, “Usawa na Haki kwa kila mtu,” wakiwemo
wapenzi wa jinsi moja ambao hapa Barani Afrika wamekuwa wakikabiliwa na
sheria kali.
Papa Francis alichaguliwa kuongoza Kanisa Katoliki Machi mwaka 2013.
Kwa miaka miwili sasa, amekuwa “MWAKILISHI WA MWANA WA MUNGU
DUNIANI”(Vicar of Jesus, Vicar of the Son of God?)naam, Vicarius
Filiidei! akijiungamanisha na masikini,wanyonge na sasa amekuwa akifanya
ziara na kuwahurumia mashoga na kutaka sheria kali dhidi yao zilaaniwe.
Kufuatia hali hiyo,ziara ya Papa hapa Afrika imekuka wakati dunia ya
Jumuiya ya Kikristo ikitakiwa kumtambua Papa kama Mwakilishi wa Yesu
Kristo hapa Duniani,wakati baadhi ya watu wanapohoji mamlaka yake
wakiuliza, “Papa ni nani?”
Alihitimu Chuo Kikuu cha Buenos
Aires,Argentina shahada ya Kemia,kisha alisoma Falsafa Collegio Maximo
de San Jose Centro Loyola,kabla ya kupata shahada ya Uzamivu(PhD)katika
Theolojia huko Ujerumani.
Alikuwa kasisi Desemba 13 mwaka 1969; na akala kiapo cha upadrisho Aprili 22 mwaka 1973.
PAPA NI NANI HATA AHUKUMU MASHOGA?
Amekuwa wakiwakaribisha mashoga kanisani na watu wenye mitazamo chanya na ushoga huku akisema, “Mimi ni nani hata niwahukumu?”
Hii ndiyo kauli ya ‘Baba huyu Mtakatifu’ wa Kanisa Katoliki na msimamo
wake dhidi ya ushoga,kwamba kuwatenga watu wa tabia hii makanisani na
katika jamii ni sawa na kuwahukumu.
Naam, Mwakilishi wa
Yesu(Vicar of Jesus) hapa duniani,anapojiuliza, “Mimi ni nani hata
kuhukumu mashoga?” anaashiria zama za Kanisa la Kristo kuwabagua mashoga
zimefika mwisho.
Siku chache zijazo,maaskofu,makasisi na wachungaji watakuwa mashoga bila kificho!
Naam Dhambi ya miji ya uwanda wa Sodoma na Gomorrah itahalalishwa duniani na makanisa.
Afrika Kusini,Ufaransa na mahali pengine,tayari kuna misikiti ya
mashoga,kilichobaki ni baadhi ya mataifa ya Afrika kulegeza misimamo na
kuhalalisha ushoga kama Ulaya na Marekani.
Kenya ni nchi ya kwanza hapa Barani kumkaribisha Papa huyu,mara alipowasili juzi uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Papa huyu alimrithi Benedict XVI alipokuwa Kadinari wa Argentina
akiitwa,Jorge Mario Bergoglio,amekuwa Papa wa 266 sasa baada ya Mtume
Petro anayeitwa Papa wa Kwanza.
Kadinari Bergoglio alichagua jina
la Francis I, kufuatisha Mtakatifu Francis wa Asisi mtu anayeshabiana
naye sana kwa tabia ya unyenyekevu na kujishusha kwa watu wote.
Hivi anavyojishusha hata kwa mashoga na watu wa chini anasemwa
kujidhili(simplicity); wanasma ni ‘kwa makusudi ambayo Kanisa linatakiwa
kuondoa vizingiti vyote katika njia ya kumtangaza Bwana Yesu kwa
Dunia’.
Papa huyu alizaliwa Desemba 17 mwaka 1936 kwa baba Mario
Bergoglio na mama Regina Siyori aliyekuwa mama wa nyumbani. Baba yake
alikuwa mfanyakazi wa reli.
Waliishi Flores jirani na jiji la Buenos Aires.
Amekuwa akikwea nyadhifa kanisani tangu miaka ya 80 hadi Papa Paulo II
alipomteua Askofu wa jiji hilo kuu la Argentina Mei 20 mwaka 1992.
Alikuwa kadinari Feburuari 21 mwaka 2001.
Sasa ni Askofu Mkuu wa Rome(PAPA)ambaye amezua mikanganyiko,akiongoza
Wakatoliki bilioni 1.2 duniani kwa namna anavyoendesha mambo yake
tofauti na watangulizi wake,walikataa kuwakubali mashoga kanisani na
wale walioacha ndoa zao halali.
Mapapa waliomtangulia
walisisitiza Wakristo kufuata ‘Njia Nyembamba’ inayobinya
demokrasia,wakati huyu ni PAPA WA KUHESHIMU HAKI ZA MAKUNDI YOTE!
Hata amethubutu kuvunja itifaki za ulinzi ili awafikie watoto yatima,masikini na wanaodharauliwa na jamii.
Akiwa ziarani Marekani Septemba mwaka huu,alikutana na mashoga,masikini na wasio na makazi.
Kenya,amekutana na Waislam na viongozi wa madhehebu mengine ya dini
akiwasisitiza kufanya maridhiano(kanisa Katoliki liliwahi kugombana na
Waprotestanti sasa Papa anaomba kupatana nao na kusameheana),anasisitiza
dunia iwe pamoja na mahali salama kwa kila mtu.
Amezunngumzia utunzaji wa mazingira akiwa Ofisi za UN mjini Nairobi,Gigiri.
Anasemekana kutowavumilia makasisi wanaowanajisi watoto.Kunajisi watoto
wa kiume ni dhambi ambayo imekuwa ikiwatafuna makasisi wa kanisa
hili,huku baadhi yao wakiomba waruhusiwe kuoa bila mafanikio.
Anatishia kuwachukulia hatua kali maofisa wa Kanisa hili watakaotumia
ofisi zao kwa manufaa binafsi. Huyu ni Papa Mkali anayesemwa ndiye
Kanisa Katoliki linayemtaka kutekeleza mipango yake.
Amekuwa hata akisafiri kwa usafiri wa umma.
Hata alipochaguliwa Papa alimuita mtu aliyemuuzia magazeti kila siku na
kumwambia, “Asante,sasa nahamia mjini Rome”. Vatican city ni nchi ndani
ya jiji la Rome.
Anasemwa kukataa uhafidhina ndiyo maana anawakaribisha mashoga,huku akisema hawezi kuwahukumu!
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani,Papa Francisco,alifika pia
Washngton na kuzungumza na Kim Davis mmoja wa walio katika sakata la
mashoga na wasagaji,kufuatia Mahakama Kuu kuhalalisha mambo hayo nchi
nzima.
Makao Makuu ya Kanisa Katoliki,THE VATICAN,yalitangaza
kwamba Papa alikwenda tu kukutana na mwanafunzi wake wa zamani,Yayo
Grassi na familia yake,ambaye kwa hakika ni shoga wa Argentina(kwao
Papa;walipotezana kitambo).
Msemaji wa Vatican,Kasisi Federico
Lombardi,akasema Papa alikutana na dazeni ya watu katika Ubalozi wa
Vatican mjini Washington,kabla ya kuondoka kwenda New York.
Akasema, kufanya mikutano na watu ni kitu cha kawaida tu kwa Papa huyu,sawa?
Na akaongeza kusema,Papa kukutana na Davis kwa muda mfupi mchana ule
Ijumaa iliyopita, ilikuwa siyo dalili kuwa anakubaliana kwa vyovyote
na ushoga ama usagaji wa akina Baba na Mama Davis.
“Papa alikusudia tu kuongea na mwanafunzi wake wa zamani na familia yake,basi”,Lombardi alifafanua.
Awali.hakufafanua huyu mwanafunzi alikuwa nani?
Kisha baadaye, picha ya video iliyowekwa kwenye mitandao ikaonesha
Grassi akii ngia hapo Ubalozini,akiwa kamkumbatia mwalimu wake huyu wa
zamani(PAPA FRANCIS),kisha akamtambulisha kwa ‘mshushu’wake huyu(shoga)
ambaye tayari Papa alikwishamfahamu katika mkutano wa awali akiwa na
marafiki wachache toka Bara Asia.
Ni hapa sasa, Msemaji Msaidizi
wa Vatican,Padri Thomas Rosica,anapobainisha ni kweli huyu mwanafunzi wa
zamani wa Papa huyu alikuwa Grassi,jamaa ambaye ni shoga.
Kwa
hakika,Papa kama Kiongozi wa Kiroho,hawezi kukataa kukutana na watu
mashuhuri kama viongozi wakuu(VIPs),Halafu akaja kuwabagua wengine kwa
sababu ya dhambi zao,kama hawa mashoga.
Lakini,imebainishwa wazi,mkutano wa Papa hapa Ubalozini Washington ulikusudia kuwa wa hawa mashoga.
Kwa mfano, mmoja wa watu aliokutana nao,Davis ni Mkiristo wa Kanisa la
Mitume(Apostolic Christian),aliyejikuta jela siku tano kwa kupinga
mahakama kutoa leseni za mashoga,kufuatia Mahakama Kuu ya
Marekani(Supreme Court)kuwa imehalalisha ndoa za mashoga nchi nzima hii.
Huyu alipinga kuhalalisha ushoga wa mumewe.
Baadaye Davis aliachwa huru baada ya Jaji kuonesha kuwa mambo yake hayakuleta madhara, alirejea kazini kwake.
Mwanamama huyu,Davis akiwa na mumewe walikutana na Papa hapa nyumba ya
mwakilishi wa Papa Marekani(Nunciature)na akawashukuru hawa akina Davis
kuwa majasiri!
Papa,aliwaunga mkono hao kwa sababu ya kile
kinachoitwa, ‘Haki za Binadamu’ siku hizi ambazo kwa vyovyote ni pamoja
na kuunga mkono haki za mashoga na wasagaji wa Marekani na dunia nzima
siku hizi.
Mkutano na hawa akina Mama Davis na mumewe ulitakiwa
ufanywe sirini na Papa,hata hivyo imesemwa kila mwanandoa alifanya
mkutano na Papa kwa siri chumbani,chini ya Ulinzi Mkali wa ‘Vatican
Security’,siri hii imekuja kubumburuka Papa alipokwishafika jijini Rome.
Kwa hiyo,Marekani watu wakashangaa Papa kukutana na hawa wanaoshadidia
usagaji na ushoga,kuungwa mkono hivyo na Kiongozi huyo anayeheshimiwa
mno duniani,kama Mrithi wa Mtume Petro.
Ilikuwa iwe siri,lakini
vyombo vya habari vimefichua jambo hili la kukaa na kukubaliana na
mashoga na wasagaji wa Marekani,nchi yenye mvuto wa kutisha wa uovu kama
huu wa SODOMA na Gomorrah hapa duniani.
Balozi wa Papa mjini
Washington,Askofu Mkuu,Carlo Maria Vigano,raia wa Italia maarufu kwa
maskandali ya ‘VATILEAKS’ yaliyosababisha Papa Benedict XVI kuachia
ngazi.
Huyu Askofu Mkuu alitoa siri ya ufisadi wa mamilioni ya
Yuro hapo Makao Makuu ya Dini Kuu duniani,baadaye alihamishiwa
Washington,baada ya Benedict kuachia ngazi.
Davis alikuwa na
kampeni mahususi,na huyu Vigano akiwa anahutubu Chuo Kikuu cha Notre
Dame mwaka 2012,akisema Mtaala wa shule ulikuwa ukiunga mkono ushoga na
usagaji ambao ni kawaida na wenye afya!
Sasa kanisa linajitetea
kwamba,PAPA awaliwajua watu aliokutana nao Ubalozini kwa majina tu,wala
hakujua sana mambo yao ya ndani.
Watetezi wa kitendo hicho cha
Papa na mashoga na wasagaji wanasema,ilikuwa bahati mbaya hivi;kwani
Papa hakujua alikutana na watu wa namna gani?
Na sasa kitendo
hicho matokeo yake yamekuwa hasi hapa duniani,kwamba Papa ameanza
kucheka-cheka na mashoga na wasagaji,kwa madai ya kuheshimu,HAKI ZA
BINADAMU.
“Kama mtu hawezi kuwapa ruhusa wengine kupinga jambo kwa uangalifu,basi anapinga Haki”,Papa anasema.
Ni kama anakubali kuwaruhusu watu ‘Kupinga Amri 10 za Mungu’
zinazopinga ushoga na usagaji,kwa uangalifu.Anasema kufanya hivyo ni
kupinga haki.
Kusema hivyo maana yake ni kwamba,PAPA Francis sasa anakuwa mwangalifu kuwapinga watu wanaokubali ushoga na usagaji.
Ndiyo maana anakutana nao kwa siri na kujadili masahibu yanayowakuta hata kama ni wanandoa kama huyu mama Davis.
Huyu Papa Francis,jina hili kwa Kilatini ni Franciscus, Kiitaliano ni Francisco.
Alipozaliwa huko Buenos Aires,Argentina Desemba 17 mwaka 1936
walimwita,Jorge Mario Bergoglio,sasa ndiye Papa wa 266 wa Kanisa
Katoliki.
Ndiye Askofu Mkuu wa Rumi(Rome)na Mkuu wa nchi, Vatican City.
Ni mmoja wa Jesuits(society of Jesus)chama alichoanzisha Ignatius Loyola.(SOMA Great Controversy)
Alikwenda kusoma seminari,akapanda vyeo hadi kuwa Askofu Mkuu wa Buenos
Aires mwaka 1998,alikuwa kadinari 2001 wakati wa Papa Yohana Paulo II.
Huyu ndiye aliyemrithi Papa Benedict XVI wakati anajiuzulu Feburuari 28
mwaka 2013,alipochaguliwa na ‘Conclave,’ baada ya Moshi Mweupe kuwaka
viwanja vya St .Peters.
Jina lake la Kipapa, ni kwa heshima ya Mtakatifu Francis wa Assisi.
Huyu ni papa wa kwanza kutoka Amerika,na wa kwanza papa asiye wa Ulaya tangu Gregory III Toka Syria,mwaka 741 AD.
Hapa wanaofuatiliamsimamo wa kanisa hili kuhusu uvunjaji wa
ndoa(talaka)na mfungamano miongoni mwa mashoga na wasagaji sasa unapewa
msimamo mwepesi.
Kanisa hili lilitegemewa kupinga uvunjaji wa
ndoa na dhambi hizi za Sodoma,sasa kuna kila dalili Jamii ya Kikristo
kote Ulaya na Marekani,kuruhusu uchafu huo kuingia kanisani,kwamba ndiyo
Haki stahiki za Binadamu!
Kanisa linakwenda kushirikiana na
wakuu wa dunia kuridhia dhambi za miji ya uwanda,ili kutengeneza Uhuru
wa watu dhidi ya Mungu wa mbinguni?
Huku wakiuliza maswali, ‘Binadamu ni nani hata awahukumu wengine?’
USHOGA IRELAND
Hakuna lugha nyingine ya kusema jambo hili,ila kueleza kwamba Ireland,
nchi ya WAKATOLIKI ambao ni asilimia 87 wamekesha Jumamosi moja Mei
mwaka 2015,kushangilia Ndoa za Mashoga na wasagaji kukubaliwa nchini
humo.
IRELAND kuna watu 4,593,100 na kati ya hawa,takriban
asilimia 90 ni Wakristo wa Madhehebu ya Katoliki,wakati madhehebu
mengine kama Church of Ireland ni asilimia tatu,na mengineyo ni asilimia
tatu pia.
Sasa,Jumamosi ,Mei 23 mwaka huu 2015,katika mji Mkuu
wa Dublin watu walikesha usiku mzima wakifurahia kura ya maoni,
“Referendum” kuwapa ushindi mkubwa mashoga na wasagaji kuoana.
“YES CAMPAIGN” waliibuka na ushindi mkubwa,kuashiria sasa nchi hii
imefanya ‘MAPINDUZI’ makubwa ya Kijamii(SOCIAL REVOLUTION)dhidi ya
Bwana mkubwa Yehova,anayepinga (kupitia AMRI 10),Mashoga na wasagaji
kuoana.
Wanaounga mkono Ndoa za Jinsi moja, “Yes campaign”
wamepata asilimia 62 ya kura zote zilizopigwa,wakati “No Campaign”
waliambulia asilimia 38 tu ya kura.
Huu ni ushindi wa kishindo wa Ibilisi dhidi ya Bwana Mungu,kuhusu suala hilo la hatari hapa Duniani..
Katika Mambo ya Walawi 18:22 BWANA aliwaambia watu wake,
“Usilale na Mwanaume mwenzako kama ulalavyo na mwanamke(ngono),ni machukizo(kwa Mungu); na usilale na mnyama(fungu la 23).
Hii ndiyo DHAMBI YA MIJI YA UWANDA wa Sodoma na Gomorrah,iliyosababisha
Mungua kuangamiza miji ile jirani na Bahari Mfu(Dead Sea).
Naam,Ireland inafuata nyayo tu za mataifa mengi hapa Duniani kuhalalisha wanaume na wanaume,au wanawake kwa wanawake kuoana.
Amri za Mungu ambazo zimekuwa zikikumbatiwa na mataifa ya Bara la
Afrika, zinasema ‘Ndoa’ ni muungano wa hiari kati ya mtu mme na mtu
mke,basi.
Hata hivyo,Afrika Kusini,kupitia Katiba ya Nchi
hii,inaruhusu mashoga kuoana(Hommosexuality),na wanawake kuwaoa wanawake
wenzao(lesbianism).
Kana kwamba hili halitoshi,Rais wa
Marekani,Barack Obama na Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron,akaamuru
nchi za Afrika kubadili Katiba zao na kuruhusu ‘MAPINDUZI’ haya- social
revolution-dhidi ya AMRI ZA MUNGU!
Marekani,ushoga na usagaji
sasa ni kitu cha kawaida sana;wanaume na wanawake wanakiri kuwa na
uhusiano wa kimahaba na wenzao wa jinsi moja-same sex,hata kama si
kufunga ndoa.
Wengine wamefanyiwa Operesheni kubadili jinsi ili
waoe au kuolewa-Mungu nadhani kachokwa katika nchi hizi zinazojidai za
demokrasia.
Kichwa kimoja cha habari kikasema:
“IRELAND MIGHT JUST HAVE BECOME A GREAT LITTLE COUNTRY IN WHICH TO BE GAY!”
Ushoga sasa ni mtindo wa leo wa kuifanya nchi inayoridhia kuwa ‘Kubwa’.
Angalia,matokeo ya kura za maoni, ‘referendum’, yaliyotolewa kwa
waandishi wa habari mjini Dublin Jumamosi hiyo,yalisema kwamba kura
1,201,607 zilipenda ushoga,na ni kura 734,300 tu zilizopinga,Riona Ni
Fhlanghaile ofisa wa Uchaguzi alisema.
Tumesema awali kwamba Ireland ina watu takriban milioni 4.6.
Kwa kawaida, nusu ya watu hujiandikisha kupiga kura katika nchi
yoyote,na nusu ya ile nusu ndiyo wanaopiga kura,sasa waliopiga kura ni
milioni mbili,na zaidi ya nusu wamekubali USHOGA!
Hii ni sawa na
kusema zaidi ya asilimia 60 ya wananchi ambao wengi ni
Wakatoliki,wameunga mkono ushoga na usagaji! Hii ni kwa mujibu wa Afisa
wa Uchaguzi, Fhlanghaile.
Kampeni ya kuunga mkono Ushoga, “YES
CAMPAIGN” ilikuwa kali mno, hata watu waliotaka kuipinga,waliona aibu
wakajikuta wanapiga kura ya ‘NDIYO’kwa ushoga.Hii ni kwa mujibu wa
Gazeti la The Guardian la Jumapili, Mei 24 mwaka huu.
Nataka
nikwambie msomaji,Ireland ina watu wengi WAKRISTO(wawe Katoliki ama
wengine)ambao sasa wanaona Ushoga siyo Dhambi,ni uhuru tu na usagaji ni
poa tu!
Hata maaskofu ni mashoga.
Kwa hiyo, sheria za
Mungu zilizowatesa watu siku nyingi kuwanyima uhuru,zimeshindwa,watu
wakashangilia usiku mzima mjini Dublin.
Wanashangilia,Mungu kushindwa na sheria zake kandamizi,zinazowanyima watu UHURU na DEMOKRASIA,siyo?
Jambo kama hili la uasi dhidi ya Maagizo ya Mungu(Agano Jipya na Agano
la Kale)liliwahi kutokea katika karne ya 10 huko mjini Paris.
Watu walishangilia sana Biblia ilipokataliwa,na watu wakasema Mungu hayupo.
Ni katika kile kiitwacho -FRENCH REVOLUTION.
Ukitazama Ufunuo wa Yohana 11:8-10 kuna kitu kinachoshabihiana na kilichotokea Dublin,Mei 2015.
Mashahidi wa Yehova,Agano la Kale na Agano Jipya, ‘wameuawa’ katika mji
mkubwa uitwao kwa mafumbo, SODOMA na MISRI,maiti zao hazikuzikwa kwa
siku tatu na nusu za mafumbo,watu wakafanya dhihaka dhidi ya maiti
hizo(maagizo ya Mungu),lakini watu wa mji ‘WAKASHANGILIA’ sana,wakafanya
shangilizi,na kupeana zawadi!
Sodoma na Misri(zama za Farao)walimkataa Mungu kwa namna hii hii.
Sababu?
Ngoja. Ufunuo 11:10 husema, “Mashahidi wa Mungu”,yaani neno
lake,Biblia,Agano Jipya na la Kale, “liliwatesa” watu wote wakaao juu ya
uso wa dunia.
Biblia,inawatesa watu kuwakataza uzinzi,kuwakataza rushwa,uchafu,uongo,mauaji n.k
Biblia inayowanyima watu uhuru,inayosisitiza kuwapo kwa Mungu na sheria
zake za kuingilia uhuru wa watu,inapokataliwa,watu hushangilia sana
kama hao wa Dublin, ambao sasa wanaishi kwa uhuru,bila kitisho cha Mungu
kuchoma mji wao unaoitwa ‘Sodoma ya Siri!’
Haya niyaache kwanza.
Nataka kusema kwamba,Asilimia 62 ya wa Irish,wamechagua ushoga
kuendelea bila kitisho katika nchi yao.Mtu mume akipata mwanaume
mwenzake wakakubaliana.
“John sasa wewe ‘Wife’wangu,mimi ndiye Mume wako, hakuna ‘Michepuko’ sawa?”
“Poa tu!”
Haya, Mwajuma naye akimpata Jasinta,wanasagana,wanaoana basi!
Uhuru,Demokrasia,Haki za Binadamu,Haki za Kiraia,Mapinduzi ya
Kiraia-social revolution n.k
Matokeo ya kura hiyo yanaonesha
wakatoliki wamekataa maagizo ya Maaskofu na Kadinali waliyokariri katika
Biblia kuwa ushoga na usagaji ni marufuku!
Gazeti la The
Guardian na Shirika la Habari la CNN limesema kura nyingi za ‘NDIYO’ kwa
ushoga,maana yake ni safari ya Ireland kuelekea kinachoitwa,JAMII HURU,
Liberal and secular society.
“ to Liberalize” ni kuweka HURU(to
set free) kutoka ‘dhana’ ya kuwepo Mungu duniani, kwa sababu ‘secular’
ni kuondoa dini, ‘not religious or spiritual’ kwa hiyo WAKATOLIKI nchini
Ireland wamekataa kufuata DINI ama mambo ya kiroho yanayomhusu Mungu.
Uamuzi wa kumpinga Mungu mjini Dublin umepokelewa kwa sherehe kubwa mitaani,(the massive street party)na mashoga wa mji huu.
Jumapili,nikitazama Aljazeera na BBC World asubuhi,nikiandaa makala
hii, nikaona kwamba Enda Kenny akisema matokeo ya kura za kuruhusu
ushoga humaanisha watu wengi katika Jamhuri hii wamejisimamia,kwa siri
katika masanduku ya kura,wametoa tamko, ‘public statement!’
Jamii ya Dublin imeamua kuwaona mashoga na wasagaji kuwa ni binadamu sawa tu,na wanalazimika kupendwa.
Naibu Waziri Mkuu wa Ireland na Kiongozi wa Labour,Joan Burton akasema
watu wa Ireland wamepiga teke kali unyanyapaa na ubaguzi(wa Biblia)dhidi
ya Mashoga.
Alimnukuu HARVEY MILK,Mwanasiasa na mtetezi wa Haki
za Mashoga(LGBT rights) aliyesema, “Matumaini hayatakuwa kimya”.Sasa
yamesema huko Ireland,yalishasema Ulaya na Marekani karibu
nzima,yanathubutu kusema Afrika,Wafrika wanaonekana wagumu,kizazi
kilichozaliwa miaka ya 1960 na 70 kikiisha,ushoga unakubaliwa AFRIKA.
WATU WA VIJIJINI ndiyo bado ngome(stronghold) ya Mungu inayopinga
ushoga na usagaji,lakini watu wa mjini,hawa wanakubali mabadiliko mtu
kuvunja ndoa anavyotaka na utoaji mimba viruhusiwe tu.
Dini ya
mjini na ile ya vijijini,vimeanza kugombana.Mjini Wachungaji sasa
wamesoma sana,wametoka Ulaya na Marekani, na mambo haya MACHAFU
SANA,wameyajaza Makanisani na misikitini,sasa wanasema vijijini
hawakusoma sana hawajui dini vizuri,walikaririshwa dini ya kizamani!
Waziri wa Afya,Leo Varadkar,shoga wa kwanza waziri ndiye aliyesoma matokeo ya kura hiyo ni MAPINDUZI YA JAMII(Dhidi ya Mungu).
.Sasa wanataka iwe hivi:
“Marriage may be contracted in accordance with law by two persons without distinction as to their sex.”
Mtu akijisikia kuoana na mtu wa Jinsi sawa na yake,wewe Padri,Sheikh au Mchungaji unamkataliaje?
Mbona Mapadri wengine na maskofu ni mashoga?
Ndiyo maana Ulaya na Marekani sasa kuna misikiti na makanisa ya mashoga.
Bendera ya Upinde wa Mvua ya Mashoga ilianza kuinuliwa karne ya
18,wakati sheria ya ndoa inayomtambua mume na mke tu ilipoaza kupingwa.
Kuna picha nyingi za mashoga na wasagaji wa Ireland wakibusiana
hadharani kuanzia Jumamosi usiku.
“The battle is not over. There are countries throughout Africa and Asia in which it is terribly dangerous to be gay,”
Norris ameisema Afrika na Asia kuwatisha wapingamashoga,kwamba sasa
vita imeanza,Ole wenu Afrika,ambako mtu kuwa shoga eti ni issue...
“It’s wonderful. It’s a little bit late for me … I’ve spent so much
time pushing the boat out that I forgot to jump on, and now it’s out
beyond the harbour on the high seas. But it’s very nice to look at.”
Hii ni kauli ya mashoga wakiona bado kitambo Dunia nzma itaimba kishoga,itatembea kishoga,ngoja tu.
Kwa ushindi huu,mashoga wamesema Vatican imepigwa mweleka mkali,bado wengine,Waislam au maprotestanti.
Vijana sasa wameamua kuondoa dini na Mungu mwenye dini katika akili zao.
Kukubali ushoga eti ni LOVE AND EQUALITY.
Wengi lazima kukubali mambo haya.
Kwa kifupi,ushindi huu ni ‘BIG MESSAGE’ dhidi ya wanaopinga ushoga,ni ‘sweet victory’ dhidi ya Mungu na watu wake.
Biblia na Vitabu vingine vitakatifu vinavyopinga ushoga,vimepigwa kumbo
kwa ushindi wa kishindo,bila shaka Mungu anashika tama,na watu
wampendao wanashangaa kuona shangilizi za Dublin juzi zimefika hadi Dar
es salaam,Mwanza na Arusha.
VITA BADO MBICHI, wakristo,waislam changamkeni mkainue vichwa vyenu juu.
0 comments:
Post a Comment