Marekani yaidharau Biblia

    Na Conges Mramba
BAADHI ya wagombea Urais wa Marekani kupitia chama pinzani cha Republican,wamesema kitabu kitakatifu,Biblia ni ‘filamu tu ya kufikirika’ iliyojipatia umaarufu;na aslani haina ukweli wowote!
Donald Trump, anayewania kuteuliwa na chama hicho kuwa Mgombea Urais mwakani,amemkosoa Mgombea mwenzake kupitia chama hicho,ambaye ni muumini wa Madhehebu ya  wa-Adventista wa Sabato,Ben Carson, kwamba Biblia anayotumia kufanya kampeni si chochote si lolote bali,ni filamu iliyopata sifa tu, “Great Movie”.
Alikuwa akizungumza  katika mahojiano na David Brody wa Shirika la Utangazaji la Christian Broadcasting Network, Septemba mwaka huu,akasema Agano la Kale na Jipya(Biblia yenye vitabu 66) ilitokana na Kilatini na Kigiriki cha zamani, “Biblia” maana yake, “Vitabu” ama Kitabu.
Trump,alikuwa kama anajibu mapigo baada ya Ben Carson kujitetea kuhusu kukosa uzoefu wa kisiasa, akajifananisha na Nuhu alivyokuwa hana uzoefu wa kazi ya uselemara,lakini akaja kujenga safina iliyokiokoa kizazi chake katika gharika(Tazama kitabu cha Mwanzo sura 6-9).
Taaluma hiyo ya Ujenzi wa Safina hufananishwa na ile Wazungu waliyotumia kujenga meli kubwa ya Fahari iliyozama mwaka 1912 huko Uingereza, Titanic. Meli kubwa ya Titanic ilizama huko Bahari ya Atlantic.
Tuijadili kidogo Titanic.
Titanic, iliitwa “The Unsinkable” kwa sababu ilithibitishwa kutozama kwa namna yoyote.
Basi,ilizama kwa sababu ya Ibilisi na maajenti wake Freemasons.
Saa nne na dakika 20.
Ni usiku wa manane wa Aprili 15, mwaka 1912. 
Hukuwepo na mimi sikuwepo, wakati huo-imepita miaka 103 kamili.
Titanic ilianza kupotelea katika mawimbi makali ya Atlantic.
Ilikuwa meli ya fahari sana kupita zote wakati huo,iligonga Mlima wa Barafu,ikaanza kupoteza mwelekeo wake.
Jumla ya watu 1,503 hatimaye walikufa katika ajali ile ya kihistoria, na kulikuwa na majeruhi wengi.
Ajali mbaya zaidi ya meli duniani ni ya Feburuari 26,mwaka 1916 meli ya Provence ya Kifaransa ilizama Mediterranean na kuuaa 3,100.
Kwanini haikumbukwi? Hii nayo ‘cha mtoto’.Uchina waliwahi kufa watu 6,000 katika ajali ya meli mwaka 1948,lakini watu hawaambiwi haya,isipokuwa Titanic tu.
Meli hii Titanic Unsikable,ilikuwa na uzito wa tani 46,500, ilianza kuzama polepole katika muda usiopungua saa tatu hivi.
Iliundwa imara sana,lakini ‘Unsinkable’ ilizama na kukomesha kiburi cha watu cha utajiri.
Ilikuwa na kimo cha futi 883.
  Jioni, Aprili 14 mwaka huo 1912 meli hiyo ikiwa safarini baharini Atlantic ilikuwa ikipasua mawimbi shwari kabisa.
Ilikuwa ikienda jijini New York, Marekani na ilitokea Southampton,Uingereza. 
 
Meli hii iliambiwa kwamba baharini kulikuwa na mabonge ya barafu, hawakusikia.

Ni hapa tunapoambiwa,Nahodha wa meli alipewa maelekezo kuwazamisha watu fulani waliokuwemo melini,kwa sababu ambazo wao Freemasons walizijua.
Kama maili 20 hivi nyuma ya Titanic kulikuwa na meli nyingine ikija-CALIFORIAN- ikazima injini zake,ikichelea kugonga milima ya barafu na kuvunjika kisha kuzama.
Titanic waliziba masikio.
Ni kawaida kwa Aprili na Mei baharini kuwa na milima ama mabonge ya barafu makubwa na marefu mno.
Mchana saa 5:40 tayari Titanic ilikwishapinduka na ijini zake zilikwishaipeleka harijojo.
Kulikuwa na meli nyingine(The White Star Line) ya kuratibu safari za Titanic ilikuwa ikikatisha bahari ya Atlantic,haikufua dafu ili kuzuia Titanic isizame,maana ilikuwa kwa maelekezo ya Freemasons.
Angalia, abiria waliambiwa meli ilikuwa inazama,wakakataa kuingia katika boti za uokozi.Waliendelea kucheza muziki mtamu na kukamata ‘Kilaji’ tu, wengine walifunga ndoa humo-walipuuza onyo. 

Wanafananishwa na wale wa zama za Nuhu na wale wanaodharau kuwepo Mungu.
Niliwahi kuona Filamu moja kwamba kulikuwa na maharusi mle,mmoja akafa mwingine akanusurika, Titanic ilikuwa na starehe zote ndani, ndiyo maana watu walioambiwa wajiokoe wakakataa. Hawakuamini “Unsinkable” ingezama hata siku moja.
Wanaume walikataa kupanda boti za uokozi wakasema wanawake na watoto kama waliogopa basi wapande hizo boti, “Haitazama!’ walisisitiza.
Walisalia ndani ya meli hii hadi ilipozama kabisa vilindini,mashua zikajaa watu wengi,wao wakakosa nafasi hatimaye.
Meli ya Uingereza, Carpathia,ilisikia mlio wa kuomba msaada ikarudi na kupita eneo lile la ajali.Iliokoa watu 712 tu waliokuwa katika zile mashua za TITANIC ILIYOKWISHAZAMA.
Eneo la ajali hii ni karibu na Pwani ya New Foundland. Hii Titanic-white star-nyota nyeupe ilikuwa ya Uingereza,na ilizama kwa maelekezo ya Freemasons,kulikuwa na MATAJIRI ambao ilikuwa hapana budi wafe kama Freemasons walivyotaka,nahodha alipewa agizo.

 Sijui unaelewa?
Meli hii inaacha simulizi, naomba mtafute habari zake, msinisumbue kwa maswali.Titanic inafananishwa na kuzama kwa dunia hii,watu wanaambiwa ajali inakuja,hawasikii ya wahubiri.
Tazama Luka 21:35 utaona zama za Gharika ya Nuhu. Duniani kuna vita siku hizi Luka 21:9,10 na ni vita kuu ya dunia inayoongelewa hapa hadi Luka 21:11
Simulizi hii ya Biblia  leo hufananishwa na Titanic iliyozama mwaka 1912 kama tulivyoona.

CARSON CHIZI?
Ben Carson, mtaalamu bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na magonjwa ya akili,amekuwa akidhihakiwa kwa kauli yake ya kutumia mifano ya Biblia,kitabu kinachofananishwa na hadithi za  kale za uongo za kujitungia(Myth),ambazo hazibebi uhalisia wa maisha ya mwanadamu siku hizi.
Trump ambaye anaona Biblia kama kisasiri(novel)alisema kitendo cha Benjamin Carson kujifananisha na Nuhu wa Biblia siyo kichekesho,bali anataka kusema kwamba,kama Mungu alivyomtuma Nuhu kuanzisha maangamizi kwa binadamu(gharika),basi sasa amemtuma Ben Carson kuwa Rais Marekani!
Wamerekani wanaamini sana teknolojia na falsafa za watu kama Charles Robert Darwin,mwasisi wa dhana ya uibukaji, “Big Bag Evolution’ na mawazo ya Mungu kutokuwepo,au kama yupo eti hana mamlaka na utawala wa dunia.
Akasema,ni kama kutumia hadithi za kufikirika za Biblia na akili za watu wanaoshika imani kupita kiasi kama huyo Carson aliyewahi kuandika kwamba Uibukaji(evolution)ulihamasishwa na Shetani.
Wagombea Urais wa Republican sasa wanatumia ‘hadithi za kufikirika’ ndani ya Biblia kama kitabu kilichofanikiwa kukaa millennia nyingi tangu nchi za Mashariki,Ulaya na Marekani na kughubika akili za watu wakazishika.
Katika mitandao ya kijamii,David Sirota,akasema Wamarekani sasa wanaishi katika unafiki wa kutisha wa dunia wanaozungumza katika lugha ya kutia mashaka,badala ya kusema watu wanachofikiri.

“Watu wote wanafanya kinyume cha wanachohubiri makanisani na misikitini,tunajidanganya nafsi zetu katika kusaka fedha..”alisema mchangiaji huyo wa kauli ya kuibeza Biblia.

Akasema hata serikali ya Marekani inatafuta pesa,Mabenki ya Wall Street, matajiri wenye pesa Marekani wanasaka pesa tu
Hata maadili mema ya Biblia yalishasahaulika,Amri 10 za Mungu zimetupwa,ni maneno katika makaratasi yanayoitwa,Biblia.
Akasema, “Kama tungekuwa waaminifu kwa Biblia,tungekwishaacha vita visivyo na faida(duniani),tungeacha kutafuta pesa,badala yake tungeitunza nchi yetu(Marekani/,watu wake na  kudhibiti deni letu kubwa kwa nchi za nje”,alisema mchangiaji huyu katika twitter.
Akasema yeye aonavyo,Biblia ni kama kitabu tu cha kukuongoza namna ya kuishi ,na kamwe siyo kitabu kilichoandikwa na mkono wa Mungu,watu watakwambia maneno mengi ya Biblia wakati hawajui hata maana yake!
Akasema watu wawe makini na Biblia,na wasiwaamini wachungaji.
Amesema anaamini kuwepo Mungu,lakini kila mtu anahaki ya kuchagua kuwa mwema au mwovu,lakini mwisho wote watarudi kwa Mungu huyo huyo,akawaambia Marekani kuwa macho na akina Ben Carson washika dini kupita kiasi waliokosa akili,wanaonga’ng’ania hadithi za Biblia.
Wanasema Mungu aliyedharau watu baada ya kuwaumba,akamtuma mtu wa miaka 600,Nuhu kutengeneza Safina kwa karne moja,akaleta gharika ya maji kwa siku 40 usiku na mchana,hadi safina ikatua katika mlima Ararati(Uturuki ya sasa),akaokoa wanyama wawili wawili,ndege,wadudu,mijusi n.k na anasema hataua tena watu,kwamba alileta upindi wa mvua kama ishara ya suluhu,hataua waovu tena!
Huu ni msimamo wa Wamarekani hawa sasa wanaopinga Biblia na unabii wake.
 Wanyama walioingia safinani zama za Nuhu walikuwa  takriban 45,000 wakati binadamu waliosikia sauti ya Nuhu walikuwa jumla wanane wa familia moja tu,miongoni mwa wakazi hao wa dunia takriban bilioni 11 zama hizo walioangamizwa na gharika.
Leo,dunia ina watu bilioni 7.1.
“Zaidi ya watu bilioni 11 walikataa wokovu zama za Nuhu,wakaangamizwa kwa gharika,wakati watu wanane wakikubali”,na jambo hilo linazamwa kama hadithi za kutunga,za Mungu kuangamiza mabilioni ya watu kwa kutumia majanga kama Katrina huko Amerika.
Sasa,Bobby Jindal na Rick Perry,wanasema majanga ya asili kama Katrina  naJoplin huko Missouri, yaliyoua maelfu ya watu,yameletwa na Mungu huyu wa akina Carson, sasa kwamba “Mungu huyo mkatili ndiye amewapa haki Wakristo kama Carson kuitawala Marekani?”
Wanajiuliza Wamarekani.

Wamarekani wamekataa kuiamini Biblia hii, wanasema inawasaidia kuishi tu kwa kutumia mashauri yake,kwani wengi wamelelewa kuwaamini akina ‘Father Christmas’ ,Santa Claus, na wanamwona Yesu kama wa kufikirika tu,hawaoni sababu kuendelea kuamini na kusumbua nafsi zao kwa imani hizo!
 Za kufikirika!
Hata hivyo,Biblia katika Ufunuo wa Yohana 13:11 inasema Marekani(Mnyama mfano wa mwanakondoo aliyeinuka bila vita huko Bara la Amerika),angebadilika na kusema kama asemavyo Shetani.
Wanazuoni wa Biblia wanasema hawashangazwi na Wamarekani kusema Mungu hayupo,kisha kuwa na mashaka na Biblia kwamba ilitabiriwa miaka 1680 kabla ya Marekani kupata uhuru,kwamba Wamarekani na serikali yao wangetilia shaka kuwepo kwa Mungu na uhalali wa Biblia Takatifu.
Mamilioni ya Wamarekani ni Wakristo wa Ki-Protestanti waliokimbia vita Ulaya katika karne ya 16.
 Huyu,Ben Carson Jumatatu iliyopita alitoa kauli nyingine iliyowachefua wa-Misri,kwamba ma-Piramidi yaliyojengwa miaka takriban 4,500 iliyopita,yalijengwa na Yusufu kama maghala ya kuhifadhia nafaka.
Wa-Misri wanaamini mapiramidi yalijengwa kama makaburi ya ma-Pharaoh

Majengo haya yaliyodumu kwa millennia nne-unusu,sasa yanasimuliwa katika harakati za kuwania uteuzi wa Republican Marekani,hadi kusababisha hata Misri kumdharau Carson kwamba ameacha Udaktari wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo,sasa anarukia Urais wa Marekani huku akisema-sema maneno ya kukariri Biblia(kitabu cha Mwanzo).
Majuma mawili yaliyopita,Carson alisimamia imani yake kwamba, “Mapiramidi ya Misri yalijengwa na Mtu Mkuu wa Biblia,Yusufu ili kuhifadhi nafaka zama zile za miaka ya njaa,badala ya kukubaliana na wanasayansi kwamba yalikuwa makaburi ya ma-Pharaoh.
Associated Press limesema Mkuu wa sekta ya Mambo ya Kale katika wizara ya Mambo ya kale,Mahmoud Afif,alijibu kusema kauli ya Ben Carson haina ithibati yoyote(siyo sahihi), ni dhana tu kuhusu mapiramidi,ni kauli zinazofanana na wanaosema yalijengwa na watu toka bara lililopotea.
Kuna video imewekwa kwenye mitandao Jumatano iliyopita na Buzzfeed News ikisema Carson alitoa  dhana hiyo miaka 17 iliyopita huko Chuo cha Michigan kinachoongozwa na wa-Adventista wa Sabato.
Katika video hii,Carson anasema, “Kwa mawazo yangu binafsi ni kwamba Yusufu alijenga Mapiramidi ili kuhifadhi nafaka”.
Alikuwa akizungumza kuhusu Agano la Kale linavyozungumza habari za Yusufu akitabiri miaka saba ya njaa katika Ikulu ya Pharaoh wa Misri,akimshauri kuweka akiba ya chakula(Mwanzo  sura 39-45).
Hii ndiyo kauli ya Ben Carson kwamba mapiramidi yalijengwa na Yusufu(Joseph)kwa nia ya kuhifadhi nafaka.
Akasisitiza, “Naamini biblia kama watu wengine wafanyavyo,na sioni kama ni ujinga kufanya hivyo ingawa maendeleo ya kisekula yanazidi kutucheka tunaoiamini,na tuko radhi kukaribisha dharau hizo”,  Benjamin Carson alisema.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright ©2015 KIRUMBA ADVENTIST CHURCH