Kwanini waovu wanapendwa na kulindwa sana na Mungu kuliko Wema?
• Vyombo vya ghadhabu vinaruhusiwa kutekeleza agenda zake!
Na Mwandishi Maalum,Kirumba
MKURUGENZI wa Vijana,Muziki na Chaplensia katika Union ya Kaskazini mwa
Tanzania(NTUC),Pr.Elias Kasika, amewataka wa-Adventista wa Sabato
kushukuru na kustahimili mema na mabaya yanayowatokea,kwa kuwa Mungu
anaruhusu kila jambo litokee kwa makusudi ya wokovu.
Akizungumza
katika Ibada maalum ya shukrani kwa Mungu katika kanisa la wa-Adventista
wa Sabato Kirumba Jijini hapa, Novemba 28 amesema kwamba haiwapasi
wanadamu kumlaumu Mungu kwa kuwa waovu wakiwemo mafisadi wanalindwa na
Mungu kuliko watu wenye haki.
“Wabaya wanalindwa na Mungu hata
watakapomaliza kufanya kazi yao ya ubaya,maana waongo na wadanganyifu
kama Yakobo walipendwa sana na Mungu kuliko hata waaminifu kama
Esau”,alisisitiza Pr.Kasika huku akikariri Biblia takatifu katika kitabu
cha Mwanzo,Warumi na. Zaburi.
Akawashauri wenzi wa ndoa kumshukuru Mungu hata ndoa zao zinapoingia katika machafuko,ili agenda ya Mungu ipate kutekelezwa.
Hapa,Pr.Kasika alikuwa akikemea tabia ya watu kutengana ama kuachana na
wenzi wao wa ndoa kwa kisingizio cha ukatili,ubaya na hiana miongoni
mwao.
Akasema pia kwamba hata wanasiasa wanakasirika na kuiingiza
nchi yetu katika vurugu kwa kushindwa kutambua kwamba Mungu ndiye
atawalaye katika dunia,na agenda zake zinapaswa kutekelezwa wakati wa
Pambano kuu baina ya ubaya na wema.
“Kaini alikuwa chombo cha
ghadhabu,alipewa fursa kutenda mema akachagua kumuua nduguye Abeli
aliyekuwa mwema,lakini bado Mungu alimwekea ulinzi ili asiuawe.Watoto wa
Kaini Mungu aliwalinda na kuwapa ujuzi na vipawa vya muziki wa hali ya
juu na uwezo wa uhunzi”,Pr.Kasika alisisitiza.
Amehoji kama wataalam
wa teknolojia ya hali ya juu wote ni waaminifu,lakini akasema Mungu
huwabariki hata waovu wanaofanya maajabu katika dunia leo, hata hivyo
waaminifu wa Mungu wanapaswa kushukuru kila jambo.
“Kama watu
waaminifu hawataki kushukuru kila jambo,basi huenda wanaweza kuliacha
kanisa wa wakaamua kuasi”,amesema,huku akieleza mateso aliyopata Paulo
wakati alikuwa mtumishi mwaminifu wa Mungu.
Amesema pia kwamba,wala
si ajabu kwa watu waaminifu wa Mungu kupata ajari,kufa au kuvunjika
miguu wakiwa katika kazi ya Mungu,kwa kuwa vyombo vya
ghadhabu(uovu)vimeruhusiwa kuendelea kufanya kazi duniani.
Akahoji,
‘Ni wangapi watakaomshukuru Mungu katika mabaya yaliyotokea? Je,kama
wewe ni mume au mke,utakwendaje kumshukuru Mungu kwa sadaka za shukrani
kama hujamsamehe kwa mabaya aliyokutendea?”
“Pendo la Mungu
linakuongoza kwa kukuumiza ili ufikirie kuungama,siyo kulaumu na
kushindwa kumsamehe mwenzako aliyekuumiza!” Pr. Kasika alisisitiza.
Baadhi ya wageni waliohudhuria katika ibada ya jana Kirumba ni pamoja na
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza,Miraj Mtaturu, Mbunge wa
Ilemela(CCM)Angelina Mabula,Mwenyekiti wa Jimbo la SNC la wa-Adventista
wa Sabato,Pr.Zadock Butoke,Mkurugenzi wa Afya wa NTUC,Dk.Silas
Kabhele,Mkrugenzi wa Mawasilano wa SNC,Pr.Beatus Mlozi ,viongozi
wastaafu wa serikali na madiwani mbalimbali katika jiji la Mwanza.
Akitoa shukrani,Katibu wa CCM mkoani Mwanza,Miraj Mtaturu amesema Kanisa
la wa-Adventista wa Sabato ni sehemu ya Jamii ya wa-Tanzania
wanaopaswa kuthamini umoja.
Amesema kuwa kiongozi wa umma ni kuwa
mtumishi wa Mungu katika sekta za umma,akaomba kanisa kuwaombea kwa
Mungu,kwa kuwa unapogusa maslahi ya watu wabaya ambao ni wachache
kulinganisha na wengi wabaya.
#SHARE NA WATAKATIFU WENGINE WA BWANA
0 comments:
Post a Comment